MJAMR

Uchanganuzi Linganishi Wa Malezi Ya Watoto Katika Michezo Ya Kuigiza Ya Kigezi Universal Actors Na Ya Jamii Halisi

Karuhanga Deusdedit, Dr Beverlyne Asiko Ambuyo PhD


Abstract

Katika tasnifu hii mtafiti ameonyesha malezi ya watoto na jinsi yanavyoshughulikiwa na wahusika katika michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors ambayo ina mkusanyiko wa michezo ya kuigiza ya wahusika mbalimbali ambao ni wa kabila ya kikiga. Michezo hii imechangia pakubwa katika malezi ya watoto katika jamii ya Wanyankore. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni ambayo ni: Kubainisha na kuchanganua vipengele mbalimbali vya kimtindo ambavyo vimetumika katika michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors, Kuchunguza maudhui yanayojitokeza katika michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors, Kutathmini dhima ya michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors katika malezi bora ya watoto na jamii halisi. Utafiti huu umeonyesha kwamba watoto wana changamoto nyingi katika jamii ambazo ni lazima hatua ya dharura ichukuliwe ili kuokoa kizazi kijacho. Mtafiti ameshughulikia michezo mitano ya kuigiza ambayo alichaguliwa kwa kutumia sampuli lengwa, pia alikusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji, mahojiano, hojaji na upitiaji wa nyaraka na data ilichanganuliwa kwa mbinu ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uamilifu. Kwa mujibu wa Wallace na Wolf (1980), nadharia ya Uamilifu iliasisiwa na wanasosholojia Auguste Comte (17871857), Harbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1923) na Emile Durkheim (1858-1917). Nadharia ya Uamilifu huzingatia kuwa fasihi simulizi ina utenda kazi katika mfumo wa jamii iliopo. Beja (2000) anafafanua kuwa Uamilifu ni kazi ambapo kitu hufanya katika mfumo wa jamii ambamo kitu hicho kimo. Dhana hii ni sahihi kwani tanzu na vipera vya fasihi simulizi ikiwemo michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors, hutegemea moja kwa moja uhusiano na michezo ya kuigiza ya utanzu au kipera hicho na jamii husika. Kwa hivyo, mwanafasihi hujihusisha na usanifu wa kazi fulani ya fasihi kwa mujibu wa utendakazi wake katika jamii. Kwa mujibu wa nadharia hii, fasihi simulizi ina jukumu la kukidhi matakwa ya jamii kulingana na tabia na kaida za wanajamii. Dhana ya michezo ya kuigiza ya fasihi huonesha dhima zinazotekelezwa na utamaduni au tanzu na vipera research.miu.ac.ug/publications 14 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 14-46 vya fasihi simulizi kulingana na muelekeo wa jamii husika. Baada ya kufanya utafiti huu kwa kina, mtafiti aligundua kwamba ni kweli watoto katika jamii tofauti huwa na changamoto sawa kama vile kujiunga na vikundi vya vijana wenye uonzo wa maadili na tabia nyingine mbovu kama kuvuta sigara uwizi na ukahaba. Utafiti huu utakuwa wa muhimu katika uwanja wa fasihi kwa sababu utawatia hamu watafiti wa baadaye kutaka kuvumbua masuala yanayozingatiwa katika malezi ya watoto katika ya kuigiza mingineyo. Utangulizi Kigezi Universal Actors ni kundi ambalo lilianzishwa na Bw.Abrahamu Rukanga katika mwaka wa 1980. Lengo kuu la kundi hili hadi leo ni kuburudisha na kuhamasisha jamii kuhusu mambo mbalimbali haswa mambo ya familia na utunzaji bora wa watoto. Hapo mwanzoni, kundi hili lilikuwa likiitwa "Kinimba" baadaye likabadilishwa na kuitwa Kigezi Universal Actors katika mwaka wa 2000 ambapo lilikuwa kundi mashuhuri la kuburudisha na Kuigiza hasa visa kuhusu utunzaji bora wa watoto. Baadhi ya michezo ya kuigiza waliyoanza nayo ni kama vile; Tindarwesire, Baryanengwe na Omwaana w’abandi. Kundi hili linapatikana katika mkoa wa Magharibi wilayani Kabale nchini Uganda. Mbali na Abrahamu Rukanga, waasisi wengine ni kama vile Elias Rutamirika, Sunday Sam na Elisha Rukanga. Michezo hii ya kuigiza imeenea na kusambaa kote katika mkoa wa Magharibi na mikoa jilani kama vile sehemu za Lyantonde na Masaka katika mkoa wa Uganda-kati. Michezo hii imechagia pakubwa katika kuhamasisha jamii kuhusu uzingativu wa tabia mwafaka katika jamii. Kama lengo lao kuu, Kigezi Universal Actors wamezidi kutunga michezo ya kuigiza kama: Kamuhagama, omuntu w'eishokye, Akamigano ka rukundo, Buri mbuzi aha nkondo yayo n’Orweshigikyire. Michezo hii inajumulisha masuala ambayo hulenga jamii ya kisasa hasahasa maisha ya watoto. Jamii ya kisasa ina vijana ambao wana uozo wa maadili kama vile kututa sigara, kuiba, ukahaba, kutoheshimu wanaowazidi umri, kukataa kufanya kazi za nyumbani nakhadhalika. Kundi hili la Kigezi Universal Actors lina michezo ya kuigiza yenye kushughulikia masuala mapana katika maisha ya mwanadamu. Kuna michezo ya research.miu.ac.ug/publications 15 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 14-46 kuigiza kuhusu mazingira, unafiki, ufisadi, ubinafsi, mapenzi, ndoa, utaifa, msako wa nafsi, ulemavu, mauti, falsafa kuhusu maisha, nasaha, maadili, malezi na kadhalika. Kwa hiyo, huenda michezo ya kuigiza ina uwezo wa kuwaonya, kuwaelimisha, kuwatahadhalisha, kuwaelekeza na kuwakosoa katika ujumbe uliomo kwenye michezo hiyo. Usuli wa Utafiti. Suala la malezi ya watoto limekuwa likisisitizwa katika Nyanja tofautitofauti hasa kisiasa na kijamii. Kisiasa, viongozi wamekuwa wakijali malezi na maisha ya watoto na hii ndiyo sababu kunakuwa na afisa kwa kamati za vijiji anayeshughulika na masuala ya watoto. Kijamii, kila familia ina wajibu wa kuadilisha watoto. Hali ya malezi ya watoto pia imekuwa ikisisitizwa katika michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors ambapo wahusika wana na visa vinavyobeba vipengere vya watoto. Jamii mbalimbali zina kwa muda mrefu zimejaribu kutibu watoto wao kimaadili kwa ajiri ya kujenga vizazi vyenye manufa kwa jamii, sio majambazi ambao hupingamiza maendeleo na mwelekeo wa jamii. BAKIZA (2010) wamelifasili neno hilo kwa kusema kuwa mtoto ni “Mtu mwenye umri kuanzia siku moja hadi miaka kumi na nane au mtu aliye chini ya umri wa wazazi
Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research

Cite This Article

Karuhanga Deusdedit & Dr Beverlyne Asiko Ambuyo PhD (2023). Uchanganuzi Linganishi Wa Malezi Ya Watoto Katika Michezo Ya Kuigiza Ya Kigezi Universal Actors Na Ya Jamii Halisi. Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research, 2(7). https://journals.miu.ac.ug/pages/article.php?article_id=1017

More in This Issue

View full issue →
31
Impact of Irish Potato Growing to the Livelihood of Farmers Acase Study Buhara Sub County Kabale District
Oshabohebwa Fortunate, Dr Arinaitwe Julius, Dr Ariyo Gracious Kazaara
post-harvest farmers Irish potato growing and productivity
32
Impact of Social Media Marketing on the Business Performance a Case Study of Restaurant and Hotel Businesses in Namungoona.
Muwonger Damasus, Otim John William, Akampurira Sarah
social media marketing business and performance
33
Impact of Sugar Cane Growing to School Drop Out in Busoga Region: A Case of Iwemba Subcounty, Bugiri District.
Birungi Juliet, Asiimwe Isaac Kazaara, Dr Arinaitwe Julius, Ojok Alex
sugar cane growing and school drop out
34
Impact of U.S.E Program Oncommunity Development. A Case Study of Nebbi Municipality
Awekonimungu Priscilla, Akampurira Sarah, Amanya Gibson
girl child education U.S.E and community development
35
Implications of Deforestation on Environment Management in Busitema Sub County, Busia District
Kasenene Aisha, Mayanja Moses, Ojok Alex
Deforestation wildlife environmental management and biodiversity