MJAMR

Uchanganuzi Wa Makosa Yakisarufi Na Athari Za Kakatika Matokeo Ya Wanafunzi Wa Kiswahili Chuoni Metropolitan Magharibi Mwa Uganda

Karuhanga Deusdedit, Dr. Beverlyne Asiko Ambuyo


Abstract

Utafiti huu ulichunguza athari za makosa ya kisarufi katika matokeo ya wanafunzi wa Kiswahili Chuoni Metropolitan Magharibi mwa Uganda Jijini Mbarara Suala la utafiti ni kwamba kumekuwa na matokeo mabaya katika mitihani ya wanafunzi wa Kiswahili kulingana na ripoti na rekodi za ofisi ya msajili wa Chuo Kikuu cha kitaifa cha Metropolitan miaka ya 2018 hadi 20121.Kwa hivyo utafiti huu ulifanywa kwa azma ya kubaini athari za makosa ya kisarufi yanayowapelekea wanafunzi wa Kiswahili kupata matokeo mabaya katika mitihani yao. Madhumuni ya utafiti huu ni kutambulisha na kuainisha makosa ya kisarufi yafanywayo na wanafunzi wa Kiswahili na kudhihirisha athari za makosa ya kisarufi katika matokeo ya mitihani ya Kiswahili Chuoni Metropolitan.Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uchanganuzi Makosa iliyoanzishwa na (Corder1969), Maswali yaliyoongoza utafiti huu ni: Je, ni makosa ya aina gani katika mitihani yafanywayo na wanafunzi wa Kiswahili Chuoni Metropolitan? Je, makosa ya kisarufi yana athari gani kwa matokeo ya wanafunzi wa Kiswahili Chuoni Metropolitan? Katika upeo, utafiti huu ulichanganua makosa ya kisarufi na athari zake katika matokeo ya wanafunzi wa Kiswahili Chuoni Metropolitan .Kundi lengwa katika utafiti huu ni wanafunzi wanaojufunza Kiswahili Chuoni Metropolitan pamoja na wahadhiri wao. Wanafunzi mia moja na watano na wahadhiri wawili ndio waliteuliwa kuchunguzwa katika utafiti huu ambapo athari za makosa ya kisarufi katika matokeo ya wanafunzi yalibainika. Hojaji na uchunguzi shirikini mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji wa data. Data ya utafiti huu ni makosa ya kisarufi ya wanafunzi wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Metropolitan Data ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya Kithamano. Matokeo ya utafiti huu yatachangia pakubwa katika uwanja wa upataji lugha, na kadhalika utawafa wanafunzi umetarajiwa kuwafaa wanafunzi wa Kiswahili research.miu.ac.ug/publications 50 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 50-82 na walimu wao wa lugha, wakuza mitaala ya Kiswahili na watafiti mbalimbali wa lugha. Usuli wa Mada Mdee (1986) anaeleza sarufi kama mfumo wa kanuni za lugha zinazoonyesha uwezo wa lugha hiyo. Kulingana na (Mgullu 1999), Sarufi ni dhana inayojumuisha vipengele vya fonetiki, fonolojia, mofolojia, sintaksia na Semantiki. Pia Tuki (1990), inaeleza sarufi kama dhana inayoeleweka kuwa na jumla ya kanuni zinazoongoza kuongea na kuandika lugha sahihi. Kwa hivyo, kulingana na utafiti huu mtafiti anatumia sarufi kama usahihi wa sentensi na maneno ya Kiswahili. Sentensi sahihi ya kisarufi lazima izingatiwe na upatanishi wa ngeli, vivumishi, virejeshi, vibaini, vitenzi, udogo, na ukubwa nakadharika kulingana na mazingira inayotumika. Makosa ya kisarufi ni matokeo ambayo msemaji wa lugha hutamkwa au kuyandika maneno bila kufuata sheria zinazotawala lugha, ni pale lugha inapotumika tofauti na malengo hupoteza lengo na madhumuni ya mzungumzaji kwa msikilizaji wake. Kila lugha hutawala matumizi ya lugha ili watu waweze kuelewana. Kanuni hizo huweza kupeleka makosa kujitokeza na kwa hivyo kupotosha ufasaha wa lugha. Makosa ya kisarufi ni pamoja na yale ya kimsamiati na kimatamshi.Athari za makosa ya kisarufi hutokea pale ambapo msemaji wa lugha hutamka au kuandika maneno bila kufuata sheria zinazotawala lugha. Kulingana na ripoti na rekodi za ofisi ya msajili wa Chuo Kikuu cha Metropolitan Magharibi mwa Uganda zinaonyesha kuwa wanafunzi wa Kiswahili wa mwaka 2018 hadi 2020 walipata matokeo mabaya katika mitihani yao. Matokeo ya utafiti huu, yalibaini kwamba wanafunzi wanapoandika insha zao ndiyo yanayowapelekea kuanguka mitihani yao Makosa mengi ni uteuzi wa msamiati na kwa hivyo kusababisha makosa ya kimuundo wa neno na wa sentensi. Kwa mfano mtu akisema ‘ninapanda mti’ usemi huu unaweza kukanganya mtu asijue ni kupanda kupi anakokusudia. Je! ni kuotesha au ni kukwea mti ikiwa muktadha hautazingatiwa. Na wakati mwingine maana inaweza ikapotea kabisa. Na hii ndiyo kusema uandishi unahitaji ufasaha wa uteuzi wa sarufi. research.miu.ac.ug/publications 51 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 50-82 Mbaabu (2005) anaelezea kuhusu makosa yanayofanywa mara kwa mara na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii. Miongoni mwa makosa yaliyobainika ni yale yanayotokana na athari za lugha ya kwanza kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kiswahili kwa mfano mnyankore akiwa anatumia kinyankore kama lugha yake ya kwanza mara nyingi anachanganya maneno ya Kiswahili na ya kinyankore, kama neno ’soma’ analitumia kuwa “shoma” yaani hilo ni kosa la kisarufi katika Kiswahili sanifu. Wataalamu wengi katika uchunguzi wao wanaeleza kuwa licha ya athari za kimatamshi, watumiaji wengi huwa rahisi sana kutambua kabila la msemaji kwa sababu ya athari za matamshi kutoka katika lugha mama (lugha yake ya kwanza). Alibaini pia kwamba makosa ya kawaida ambayo hufanywa na watu wazima wanapotumia lugha ya Kiswahili miongoni mwa jamii za Kenya huzua athari za lugha zao za mama kwenye Kiswahili na kwa hivyo hukikosesha ladha na hata pengine kugeuza muundo wake. Kwa mnasaba huo utafiti wake uligusana na huu ambao ulishughulikia athari za makosa ya kisarufi katika matokeo ya wanafunzi wa Kiswahili Chuoni Metropolitan. Utafiti huu ulichunguza athari za makosa ya kisarufi katika matokeo ya wanafunzi wa Kiswahili Chuoni Metropolitan Magharibi mwa Uganda Jijini Mbarara. Makosa hayo ya kisarufi na athari zake katika matokeo ya wanafunzi wa Kiswahili hazijawekwa wazi. Mtafiti amebaini kwamba athari za makosa ya kisarufi yanaweza kudhihirishwa katika uwandishi wa insha na imla. Kwa hivyo, mtafiti amebaini kwamba wahadhiri
Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research

Cite This Article

Karuhanga Deusdedit & Dr. Beverlyne Asiko Ambuyo (2023). Uchanganuzi Wa Makosa Yakisarufi Na Athari Za Kakatika Matokeo Ya Wanafunzi Wa Kiswahili Chuoni Metropolitan Magharibi Mwa Uganda. Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research, 2(7). https://journals.miu.ac.ug/pages/article.php?article_id=1018

More in This Issue

View full issue →
46
Painting Illustrations on Gender Based Violence on Women’s Participation in the Development of Uganda, a Case Study of Bombo Luwero District
Alinda Rehema, Nkwasiibwe Kenneth
painting illustrations gender-based violence women’s participation
47
Product Packaging and Sales Volume of Bakery Industry a Case Study of Kiddawalime Bakery
Tabola Julius, Akampurira Sarah
product packaging sales volume and bakery industry
48
Relationship Between Public Finance Management and Corruption Practices in Uganda: A Case Study of Wakiso District Local Government.
Nimusiima Sheila, Dr Ariyo Gracious Kazaara, Dr Arinaitwe Julius
public finance management and corruption practices
49
Religious Studies and Students’ Behaviour Change in Secondary Schools: A Case of Namugoona High School, Kampala District.
Tugumisirize Bridget, Mukoyani Geophrey
Religious Education Behavior Change Secondary Schools and
50
Risk Assessment, Trust and Cashless Policy Adoption Among Suppliers of Uganda Tobacco Services Limited, Hoima Uganda
Alex Irumba, Victor Mugabi, Dr Ariyo Gracious Kazaara
risk assessment trust and cashless policy