MJAMR

Usawiri Wa Jinsia Ya Kiume Katika Riwaya Ya Msururu Wa Usaliti

Karuhanga Deusdedit, Dr. Beverlyne Asiko Ambuyo


Abstract

Utafiti huu ulishughulikia usawiri wa jinsia ya kiumme katika riwaya ya Msururu wa usaliti. Mtafiti alichanganua taswira ya mwanamme katika riwaya ya Msururu wa usaliti. Kuchanganua taswira za mwanamume katika Riwaya ya Msururu wa usaliti na Mwenda Mbatiah na ile ya jamii ya kiafrika, Kutathmini uhusiano wa mwanamume na mwanamke kimamlaka katika Riwaya ya Msururu wa usaliti., Kubainisha namna tamaduni na itikadi za kijadi zinavyochangia hulka ya mwanamme katika jamii ya Msururu wa Usaliti. Nadharia ya ubabedume iliyotokea miaka ya 1980 kupitia maaandishi ya John Gray itatumiwa. Mihimili ya itikadi za jamii, uwezo na uongozi pamoja na utamaduni ndizo zilizotumiwa katika utafiti huu.Utafiti huu ulishughulikia kazi ya Msururu was usaliti, riwaya yake Mwenda Mbatiah. Riwaya hii imechaguliwa kwa sababu ina wahusika wengi wa kiume na kike wa umri, tabaka, viwango vya elimu tofauti na kadhalika ambao wanajitambuliza na kutambulishwa na jamii tofauti tofauti. Muundo wa kimaelezo ulitumwa katika utafiti huu. Riwaya ya Msururu wa Usaliti ilisomwa ili kupatata deta. Deta iliyofanyiwa utafiti ni ile deta tu inayoshughulikia taswira ya mwanamme.Sehemu zingine riwayani hazitashughulikiwa. Deta iliyokusanywa ilinakiliwa kisha baadaye kuchanganuliwa kwa kutumia uchaganuzi wa kiuthamano ambapo programu ya SPSS ilitumiwa. Uchanganuzi uliongozwa na madhumuni ya utafiti.Utafiti huu utachangia katika kuweka msingi wa kuchanganua riwaya ya kisawhili kitaaluma kwa kujikita kwenye kipengele cha jinsia na mamlaka hasa mamlaka ya mwanamme dhidi ya mwanamke. Kazi hii itakuwa mwongozo kwa waandishi wa baadaye wa riwaya ya Kiswahili kuandika kazi nzuri kuhusu jinsia ya research.miu.ac.ug/publications 11 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 11-44 kiume kwa kurejelea jamii Fulani. Vilevile utafiti huu utasaidia wasomi kuelewa taswira mbalimbali za mwanamme na jinsi picha hizi zinavyomwathiri mwanamke. Usuli wa Mada Riwaya ni mojawapo wa tanzu za fasihi andishi ambayo ni utungo mrefu wenye wahusika wengi na unaotungwa kwa njia ya masimulizi. Fasihi andishi ni aina ya fasihi inayosambazwa na kuhifadhiwa kwa njia ya maandishi kwa mfano, riwaya, tamthilia, mashairi, hadithi fupi na kadhalika. Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kwa njia ya ubunifu kuelezea masuala mbalimbali yanayomuhusu binadamu na mazingira anamoishi. Na fasihi hugawika katika aina kuu mbili ambazo ni fasihi andishi na fasihi simulizi. Suala la uana limepewa kipaumbele miongoni mwa masuala yanayotafitiwa katika taaluma mbalimbali zinazohusu maisha ya binadamu. Majukumu ya jinsia ya kike na jinsia ya kiume ni suala ambalo linaendelea kuzua mgogoro miongoni mwa watu wa jamii mbalimbali. Tafiti nyingi zilizopo zimeshughulikia masuala ya kike. Kuna haja ya utafiti kufanywa kuhusu suala la jinsia ya kiume katika fasihi Mwanamme kote duniani amepewa hadhi ya juu kuliko mwanamke. Chanzo cha tofauti hii kulingana na Engles (1975) ni migawanyiko ya utabaka. Anaeleza kwamba wanajamii walikuwa wakiishi maisha ya ujamaa. Mabadiliko yalipotokea kukazuka mfumo wa ubabedume ulioanza kutawala mahusiano yote ya jamii. Mfamo huu ulikolea wakati kazi za waume kama ufugaji zilianza kuleta faida kuliko kazi za wanawake za nyumbani. Kulingana na Engels (Ibid), huu ndio ulikuwa mwanzo wa mwanamke kumtegemea mwananmme katika uhusiano wote wa jamii hasa wa kiuchumi. Hivyo mwanamke kuwa na hadhi ya chini huku mwanamme akiwa na hadhi research.miu.ac.ug/publications 12 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 11-44 ya juu, mshawasha huu ndio unamfanya mtafiti kuchunguza kama hali hii inajitokeza katika riwaya ya Msururu wa Usaliti. Kuhusu ulimwengu unaotawaliwa na wanaume Dehlerup (1987) anasema, ubabedume ni hali ambapo nafasi zote za utawala au uongozi na uamuzi ziko mikononi mwa wanaume yaani ni hali inayomwangalia mwanamke kama mtawaliwa na mwanamme kama mtawala.Katika utafiti huu mtafiti aliangalia hali inavyojitokeza katika riwaya ya Msururu wa usaliti. Nafasi kama vile za kisiasa kuchumi, viwandani, kidini na kijamii ambamo idadi kubwa ya nafasi za juu katika uongozi zinachukuliwa na wanaume. Bila shaka hali kama hizi zinamwacha mwanamke katika mashaka. Hiyo basi, utafiti huu ulijaribu kuangalia kama hali hii inadhihirika katika riwaya ya Msururu wa Usaliti. Moi (1985), anasema kwamba mwanamme ana sehemu ya maumbile yake ambayo ni dhahiri – uume na mwanamke hana. Freud anapomwangalia mwanamke haoini thamani yoyote kwake.Tofauti ya kimaumbile ya mwanamke na mwanamme imeangaliwa kama chemichemi ya ukinzano wa kimawazo na hatimaye kusababisha tofauti katika majukumu ya kijamii. Hali hii inampa mamlaka mwanamme dhidi ya mwanamke na kwa njia moja au nyingine kumdunisha mwanamke. Mfafiti alijaribu kutathmini ikiwa hali hii inajitokeza katika jamii ya mwandishi wa Msururu wa Usaliti. Maclennes (1998) anabainisha jinsi ambavyo masharti ya kihistoria na ya kitamaduni yanavyo halalisha mielekeo na mitazamo tofauti baina ya jinsia ya kike na kiume. Anaelezea kuwa udume hauwezi kubainishwa kama sifa ya mwanamme bali hutokana na itikadi na utamaduni wa jamii husika. Masharti mahsusi ya kihistoria yanayodhibiti imani za mme na mke katika jamii na majukumu yao tofauti huendelezwa kupitia kwa imani za kijamii, matarajio na mielekeo yao.Utafiti huu unanuia kupata ukweli wa usemi huu. Riwaya ya Msururu wa usaliti ya Mwenda Mbatiah ilishughulikiwa. research.miu.ac.ug/publications 13
Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research

Cite This Article

Karuhanga Deusdedit & Dr. Beverlyne Asiko Ambuyo (2023). Usawiri Wa Jinsia Ya Kiume Katika Riwaya Ya Msururu Wa Usaliti. Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research, 2(7). https://journals.miu.ac.ug/pages/article.php?article_id=1019

More in This Issue

View full issue →
57
The Effect of Plastic Waste on the Environment in Uganda, a Case Study of Jinja District
Alex Irumba, Kamugisha Nelson, Asiimwe Isaac Kazaara
plastic waste and environment
58
The Effects of Memorial Sites on Growth and Development of Tourism in Uganda a Case Study of Namugongo Martyrs Shrines
Niyonzima Wilber, Kamugira Apophia, Kaziro Nicholas
memorial sites growth development and tourism
59
The Government Policies and Poverty Eradication Among Women in Uganda: A Case Study of Kawempe Division, Kampala
Kyakuwa Victo, Akampurira Sarah, Turyatunga Micheal
government policies and poverty eradication
60
The Impact of Climate Patterns on the Farming Activities in Uganda. A Case of Kibibi Town Council
Mubiru Elifaazi, Balunywa Ali, Alex Irumba
climate patterns and farming activities