Journal
Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research
MJAMR
Mchango Wa Komedia Za Kiswahili Katika Ujifunzaji Wa Lugha Ya Kiswahili
Karuhanga Deusdedit
| Journal | Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research (MJAMR) |
| Volume / Issue | Vol. 2, No. 7 |
| Published | 31 July 2023 |
| ISSN | 3006-4384 |
Abstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza mchango wa komedia za Kiswahili katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kitaifa cha Metropolitan. Utafiti huu umejengeka kwa msingi kwamba fasihi yeyote kokote iwapo huchangia sana katika usambazaji na ujifunzaji wa lugha, lakini utanzu wa komedia hasa za Kiswahili, umeachiliwa nyuma na kuangaliwa kama utanzu duni katika ujifunzaji na usambazaji wa lugha ya Kiswahili. Badala yake, tanzu nyingine zimepewa nafasi ya kwanza na kusemwa kuwa ndizo zinazotoa mchango mkubwa katika ujifunzaji na usambazaji wa lugha ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya ueneaji ambayo inazingatia chimbuko la taaluma fulani na kujaribu kufuata mikondo iliyopitia hadi kufikia hali ilivyo wakati wa uchambuzi. Tasnifu hii iliongozwa na madhumuni matatu yafuatayo: kubainisha komedia mbalimbali zinazopendwa na Wanafunzi wa tarafa ya Biharwe ; kuchunguza mchango wa komedia zinazopendwa na Wanafunzi wa tarafa ya Biharwe katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili pamoja na changamoto mbalimbali zinazoukumba utanzu wa komedia za Kiswahili katika uendelezaji na usambazaji wa lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa tarafa ya Biharwe jijini Mbarara. Utafiti huu ulilenga kujibu maswali yafuatayo: ni komedia zipi ambazo zinapendwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kitaifa cha Metropolitan? komedia za Kiswahili zimechangiaje katika ujifunzaji na usambazaji wa lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Biharwe? na utanzu wa komedia unakumbwa na changamoto zipi katika usambazaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kitaifa cha Metropolitan jijini Mbarara. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka nyanjani ambapo mtafiti alitumia maskani ya research.miu.ac.ug/publications 17 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 17-34 wanafunzi wa Chuo Kikuu Metropolitan ambayo ni “White house ”, na “Altimate” yanayopatikana katika tarafa ya Biharwe jijini Mbarara. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano, hojaji na majadiliano. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya maelezo yaliyolenga kufafanua majedwali na michoro iliyopatikana katika data yake. Utafiti huu uligundua kuwa kwamba Wanafunzi wengi wanazipenda komedia za Professa Hamo. Matokeo yalionyesha kuwa komedia za Kiswahili zinachangia pakubwa katika ujifunzaji na usambazaji wa lugha ya Kiswahili miongoni mwa Wanafunzi wa tarafa ya Biharwe kwani zinawafunza wanajamii hasa Wanafunzi wa Biharwe misamiati mipya na jinsi ya kuizalisha misamiati hiyo, mtafiti aligundua kuwa uchanganyaji ndimi kama mbinu ya uwasilishaji huwafanya watazamaji kutoelewa baadhi ya mambo yanayozungumziwa na vile kuwafanya wasijifunze lugha ya Kiswahili kwa urahisi. Utafiti huu utoonyesha mchango wa komedia za Kiswahili katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Pia, utawasaidia watafiti wengine kwa kufanya kama nguzo ya kuwaongoza watakapokuwa wanatafiti jambo linalohusiana na mada hii. Mtafiti alipendekeza kwamba kuna haja ya kuanzisha uchezaji na utunzi wa komedi za Kiswahili nchini Uganda ili sanaa hii ifikie umati mkubwa wa wanajamii; kuna haja ya kuanzisha kuzionyesha hizi komedia za Kiswahili kenye vituo vya televisheni nchini Uganda ili ziwafike watu wengi na wajifunze lugha ya Kiswahili moja kwa moja na kwamba komedia za Kiswahili zafaa sana kuwekewa mashindano kwenye shule mbalimbali, vyuo na ndaki mbalimbali ili kuinua mapenzi ya wanajamii kuzihusu na kuhusu lugha ya Kiswahili na lengo la kuwafanya watoe imani potovu kuhusu kutofaa kwa lugha ya Kiswahili. research.miu.ac.ug/publications 18 METROPOLITAN JOURNAL OF SOCIAL AND EDUCATIONAL RESEARCH ISSN: 1813-4270 Vol. 2 Issue 4, July - 2023, Pages: 17-34 Usuli wa Mada Utafiti huu unahusu mchango wa komedia za kiswahili katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili miongoni mwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kitaifa cha Metropolitan jijini Mbarara. Sura hii inazingatia usuli wa mada, Tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, upeo wa utafiti, umuhimu wa utafiti pamoja na misingi ya nadharia ya utafiti. Kwa mujibu wa Habwe na Karanja, (2004), lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana. Lugha ni mfumo wa sauti nasibu na ishara za kisarufi ambazo kwazo watu wa jamii fulani ya lugha huwasiliana na kupokezana utamaduni wao. Hii ina maana kwamba lugha ni chombo muhimu cha utamaduni, lugha ni sehemu ya utamaduni na ni chombo kinachosheheni sifa za utamaduni wa jamii husika katika misamiati, miundo na matumizi ya lugha zinazohusika. Lugha hutumika kukuza utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa mujibu wa (TUKI, 2005), Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambayo hutumiwa na watu wa taifa au kundi Fulani kwa ajili ya kuwasiliana. Mahusiano ya kijamii hujengwa kutokana na historia, mazingira na shughuli za watu za kila siku na imani yao pia. Watu wa jamii moja mara nyingi husikilizana kwa lugha, mila na desturi. Misingi hiyo ya utamaduni na utamaduni wenyewe huwa ni vigezo maalum vya kumfanya mtu aitambue nafasi yake katika jamii na vilevile kutambua wajibu wake na majukumu yake, Mazrui (1986). Tamthilia ni utungo wa kisanaa ambao huweka wazo fulani katika matendo na mazungumzo (TUKI, 2004).Hivyo basi tunaweza kusema kuwa tamthilia ni utungo au mchezo wa kuigiza matendo au mawazo fulani yaliyopo katika jamii, ambapo huwa ni majibizano baina ya watu wawili au zaidi. research.miu.ac.ug/publications 19
Cite This Article
Karuhanga Deusdedit (2023). Mchango Wa Komedia Za Kiswahili Katika Ujifunzaji Wa Lugha Ya Kiswahili. Metropolitan Journal of Academic Multidisciplinary Research, 2(7). https://journals.miu.ac.ug/pages/article.php?article_id=1020
More in This Issue
View full issue →
11
12
Assessing the Quantity of Plastic Waste Transported Along Nakivubo Channel Towards Lake Victoria
plastics
KCCA
Nakivubo and recycling
13
Assessing the Relevance of Population Census to the Economic Development of Uganda (The Case Study of Nansana Municipality)
population census and economic development
14
Corporate Governance, Product Innovation, Customer Satisfaction and Shareholder’s Value. A Case Study of Selected Construction Firms in Kampala
corporate governance
product innovation
customer satisfaction and
15
Customer Perception, Customer Response and Mobile Banking Usage Within Bank of Africa Uganda Limited,
customer perception
customer response and mobile banking usage